
Soma.

Jamii yangu kwa asilimia kubwa inachukulia suala la hedhi kama suala la aibu, jamii bado inaona hedhi ni suala la binti mwenyewe bila kupewa msaada ili kuweza kuwa na hedhi salama kwa kumsaidia kuepuka changamoto mbalimbali wakati wa hedhi.
Mazingira bado si salama, maeneo mengi ya kazi, shule na hospitali vyoo si visafi, hakuna Tissue wala toilet paper na wakati mwingine hakuna maji na kubwa zaidi ni ukosefu wa taulo za kike za kujihiifadhi kwa dharura endapo hedhi itamtokea msichana bila kutarajia.
Mfano, Binti ambaye anavunja ungo kwa mara ya kwanza ambaye anaona uoga kwenda kumueleza mwalimu, anajikuta katika kuhangaika kujihifadhi anaishi kuaibika kwasababu vyoo vya shule anakuta hakuna maji, tishu,karatasi za chooni wala khanga ya dharura ya kuweza angalau kumhifadhi hadi atakapofika nyumbani na matokeo yake anaishia kuaibika mbele ya rafiki zake na watu njiani.
Maumivu ya tumbo ndio changamoto pekee inayonikumba nikiwa kwenye hedhi.
Hedhi si jambo la siri hata kidogo, nimekua nikimshirikisha sana mume wangu kwa kumuelezea kwa uwazi kuhusu hedhi hasa hedhi salama na namna ya kunisaidia kujistiri ikitokea ninaumwa sijiwezi na tuko wenyewe badala ya kusubiri hadi watu wengine waje. Lakini pia nimekua nikimsihi kuwa malezi ya watoto wetu hapo baadae ni jukumu langu na lake hivyo basi anapaswa kufahamu vyema kuhusu hedhi salama na asiionee aibu kwasababu ni AFYA.
Wasichana wadogo wanapaswa kuacha kuona aibu wanapokua kwenye hedhi, watambue kuwa wanapoona aibu ndivyo wanavyozidi kuhatarisha usalama wa Afya zao kwani watakua wanapata dalili mbalimbali za magonjwa au changamoto za kiafya zinazoweza kuleta madhara makubwa wakashindwa kuwaeleza watu wa karibu (wazazi au walezi) ili waweze kusaidiwa kwa haraka .
Ombi langu kwa mashirika binafsi na serikali ni kuona kuwa wote tunawekeza nguvu kwenye suala la hehi salama kwa kuahkikisha shule zina matundu ya vyoo ya kutosha, vyoo visafi na bora, uwepo wa maji safi tiririka, uwepo wa taulo za kike za kutosha za dharura na khanga pia ili kwa pamoja tuweze kupiga hatua katika kuhakikisha binti anakua na hedhi salama. Lakini pia tushirikiane kutoa elimu kwa walimu na wazazi waweze kujua umuhimu wa hedhi salama na namna wanapaswa kuwa rafiki kwa wasichana ili wasiwe waoga kuwaeleza changamoto zao wanapokutana nazo kipindi cha hedhi.
Hedhi imekua kikwazo kikubwa sana katika elimua ya mtoto wa kike kwani wapo wanaoshindwa kwenda shule siku 3-7 kwasababu ya maumivu makali wakati wa hedhi na wengine kwasababu ya ukosefu wa taulo za kike za kujihifadhi hivyo anaweza baki nyumbani hadi amalize hedhi matokeo yake anakua amekosa vipindi shuleni na wanafunzi wenzie wameendelea na masomo. Lakini pia sisi tunaamini #HerEducation inategemea sana afya ya msichana ambapo msichana akiwa hajui kuhusu hedhi yake (mzunguko) na namna ya kujikinga na mimba basi anaweza pata mimba bila kujua na kukatisha masomo na ndoto zake.
Sisi, Binti Salha Foundation tumejikita kuhakikisha tunaifikisha elimu ya hedhi salama kwa wasichana mashuleni na vyuoni lakini pia kwa wazazi na walezi kupitia klabu zetu (BSF Parenting Clubs) ili kuweza kuvunja ukuta na kutengeneza mawasiliano na mahusiano mazuri kati ya wazazi (baba na mama) na mabinti zao katika kuwasaidia kuweza kuwa na hedhi salama yenye kuwapa AFYA bora ya sasa na baadae.
Hedhi salama kwa Msichana/ Mwanamke ni UHAI na ni Afya bila hedhi salama hakuna uzazi salama hivyo basi tuungane pamoja kuhakikisha kuwa Hedhi salama inakua chachu ya kupunguza mimba za utotoni na vifo vya uzazi kwani binti anayejijua vizur na hedhi yake hawezi pata mimba bila kujua/kutarajia.

Jamii inayonizunguka sababu ni mjini sijasikia wakizungumzia suala la hedhi. Huwa nawaza je huko vijijini inakuwaje? Bado mitazamo ni ile ile kuwa suala la hedhi haliwezi zungumzwa mbele za watu hasa kama kuna wanaume.
Bado mazingira sio rafiki. Maana sasa mtu unatamani tu upate hedhi ukiwa nyumbani ili uweze kujisitiri. Lakini sasa hedhi ikukute mihangaikoni huko jamani na umesahau pedi, utatamani uzame chini upotee. Lakini pia hata kama unayo kupata sasa choo kisafi cha kwenda kunawa vizuri na kuvaa pedi bado ni changamoto.
Mimi binafsi ni changamoto za kiafya. Huwa naumwa sana sana, muda mwingine hata kutembea ni changamoto. Yani nyonga hizi zinauma sana. Kwa hiyo, muda mwingine hupelekea hata kupungua kwa ufanisi wangu wa kazi au kutokwenda kabisa ofisini.
Na kama nikienda basi hapakaliki ni mateso tu.
Hedhi sio siri. Binafsi mume wangu anajua hadi tarehe zangu na huwa anaenda kuninunulia pedi. Pia ofisini kwangu wanajua ni lini tumbo litaanza harakati zake za kusokota. (anacheka)
Lakini tumeweka pia pedi za dharura .
Ninachoweza kuwaambia wasichana ni kwamba Hedhi sio ugonjwa, na kila mwanamke mkubwa wanaemuona yuko Imara yawezekana anapata hedhi au ameshawahi kupata hedhi.
Hivyo wasiichukulie kama kikwazo au kuona aibu. Wasisite kuomba ushauri juu ya suala la Hedhi Salama. Na kunwa zaidi ni kuhakikisha wanakuwa wasafi muda wote hasa wanapokuwa kwenye siku za hedhi
Ombi langu kwa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali. Tuendelee kupambana kuhakikisha Binti anapewa elimu sahihi ya Hedhi salama na kuwekeza kwenye mazingira rafiki ya kuhakikisha taulo za kike zinapatikana kwa bei nafuu kwa binti wa hali yoyote ile. Mwisho kwa familia pia tuhakikishe tunalifanya suala hili la Hedhi salama kuwa la uwazi na linaloweza kuzungumzika .
Asante sana
Hili si jukumu la serikali pekee na mashirika. Ni letu sote, tuwekeze katika kuondoa vikwazo kama hivi zinavyoweza kuwa sababu ya mabinti wengi kukosa uhuru wa kupata Elimu na kushiriki kwenye masuala ya kijamii kwa kushindwa kujisitiri vyema au kuona aibu kujitokeza.
Hedhi salama ni ile ambayo mtoto wa kike atapata mahitaji yote muhimu kama pedi, maji na sehemu safi ya kubadilisha. Na atajihisi huru kuendeleza shughuli zake.
Mzunguko wa siku za hedhi kwa wanawake ni jambo ambalo mara nyingi halizungumzwi hadharani katika jamii nyingi barani Afrika kutokana na imani za kitamaduni.
Mazingira salama au kutokuwa salama hutegemea na maeneo uliyopo.
Kwa nyumbani: Ni sehemu salama kwa wanawake wengi kwasababu ya kuwepo kwa maji Safi, vyoo visafi na upatikanaji wa taulo za kike. Japo kwa wanawake wengine nyumbani si sehemu salama pia maana Kuna uhaba wa maji safi, vyoo na taulo za kike.
Hali kadhalika na shuleni, pamegawanyika pia. Shule nyingine ni sehemu salama kwa wanawake waliopo kwenye mzunguko wa hedhi na shule nyengine si rafiki kutokana na kutokuwepo kwa mazingira rafiki ya Hali yao.
Hapana si Jambo la Siri na halipaswi kuwa Siri kwasababu inahusisha afya ya wanaadamu.
Nikiwa nyumbani, baba yangu lazima ajue kwasababu yeye ndo atakaeenda "pharmacy" kuninunulia taulo za kike.
Nikiwa nje na nyumbani, Basi rafiki wa kiume lazima ajue kwasababu ataenda kuninunulia pia. Huwa sipendelei kwenda kununua pedi mwenyewe. Nafarijika jinsia "ME" ndo aninunulie. Pia ni faraja maana naona ahueni pale anavyojaribu kuvaa viatu vyangu vya maumivu ninayosikia.
Kujitahidi usafi wa Hali ya juu, unaweza kuwa kwenye mazingira mazuri ya kuwa na vyoo visafi, maji Safi kuwepo na taulo za kike nyingi Ila usipozingatia usafi hedhi yako inakuwa si salama. Badilisha pedi kila baada ya masaa7 na hakikisha unajisafisha vizuri Mara kwa Mara ili kuepuka muwasho na fangasi.
Kuhakikisha kuwepo na kupatikana kwa maji Safi kwenye maeneo yote, vyoo visafi na kuwepo kwa taulo za kike.
Kwa kuwa Serikali haiwezi kufuta Kodi kwenye bidhaa ya taulo za kike Basi tunaiomba zile kaya maskini wagawiwe reusable pads ili ziwasaidie kwa muda mrefu. Pia kwa pamoja tunaweza changia hili.
Takwimu zinaonyesha "wasichana wanakosa masomo 50 kati ya 194,vipindi 400 kati ya 1552 kwa mwaka" Mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP).
Kwa kumalizia, Yatupasa tufahamu kwamba Hedhi salama ni chachu katika kumuokoa msichana na kumpa amani na Hali ya kujiamini muda wote.

Kwa upande wa jamii ya kimaasai ambapo nimekulia tangu udogo wangu, Mila na desturi hazina utaratibu rafiki kwa mwanamke kupata hedhi salama(Hakuna pedi, maji safi pamoja na elimu yoyote inayotolewa).
Wanawake wengi wanaopata na hii hali huishia kukimbia Porini na kujifuta na majani laini pamoja na kujifunga vitambaa ambavyo ki uhalisia sio visafi na vinaweza kusababisha Magonjwa mengine.
Pia hali hii ikitokea wakati mwanamke yupo kwenye mikusanyiko watu wanamshangaa bila kumsaidia na kuona kama ana ugonjwa wa ajabu na wengine kumkejeli hivyo anakosa kujiamini mbele za watu na kusababisha matatizo ya kisaikolojia.
Jambo ninaloweza kusema kwa wasichana juu ya Hedhi salama.
-Wajitahidi kupata Elimu ya kutosha juu ya swala la hedhi ili kuweza kujihudumia vizuri hali hii inapotokea kwani kuna ambao kwa mara ya kwanza wanajishangaa na kuona ni kama ugonjwa wa Ajabu.
-Pili, Wafanye Maandalizi mapema kama kununua pedi mapema na sio kusibiri hadi hali itokee ndipo wanunue.
-Wadumishe Usafi kwa kipindi hicho kuepusha harufu ambazo husababisha kubezwa na wanaume.
Na mwisho, Kwa wadau mbalimbali, watoe Elimu kubwa hasa vijijini kwa Wazazi na watoto wa kike juu ya Hedhi salama pamoja na kutoa misaada ya Pedi vijijini.
Nyumbani Tanzania, usafi wa hedhi sio suala la kujadiliwa waziwazi katika maeneo mengi. Mara nyingi tunapata uelewa mashuleni. Wasichana wengi hubaki hawajui juu ya hedhi hadi mzunguko wao wa kwanza wa hedhi. Hawapewi kipaumbele kama hitaji muhimu la kiafya.
Hata kuzungumza juu ya hedhi ni mwiko katika jamii nyingi, hii inapelekea kutokuwa na taarifa sahihi
Ikilinganishwa na mahali nilipo, usafi wa hedhi unachukuliwa kuwa muhimu. Vifaa vinapatikana sana ukilinganisha na Tanzania, ufahamu juu ya hedhi salaam hutolewa kwa vijana na mwanamke. China, hata wakati huu wa janga la ugonjwa huu wametoa "sanitary pads" bure kwa wanawake wa vyuo vikuu na sehemu zingine zenye lockdown.
Nakumbuka kipindi fulani, nikiwa na familia na sote tulikuwa tukitumia choo kimoja, nilikuta Kama damu damu yenye mabonge chooni, nilishangazwa (baadae nilihisi ni ndugu yangu X alikuwa akipitia katika kipindi cha hedhi, ila kutokana na umri wake hakuwa amefundishwa mapema namna ya kuzingatia usafi anapokuwa katika kipindi hicho) niliwashirikisha ndugu wa kike wakubwa kumsaidia, nilihisi angejisikia vibaya mimi kumjuza.
"Hedhi kwa upande wangu si jambo la siri haswa kwa ndugu wa kike na rafiki wa kike lakini piah ni jambo la siri kwa jinsia ya kiume kwa sababu wengi wakishafahamu siku zako basi hutaka kukuchokoza kila zinapofika siku za mzunguko wako na hutumia maneno yanayoweza kukukasirisha zaidi mfano vipi mama unalimwaga?, mama Leo salama kweli, tayari nini? Na maneno mengine kadha wa kadha"

Hata kuzungumza juu ya hedhi ni mwiko katika jamii nyingi, hii inapelekea kutokuwa na taarifa sahihi
Ikilinganishwa na mahali nilipo, usafi wa hedhi unachukuliwa kuwa muhimu. Vifaa vinapatikana sana ukilinganisha na Tanzania, ufahamu juu ya hedhi salaam hutolewa kwa vijana na mwanamke. China, hata wakati huu wa janga la ugonjwa huu wametoa "sanitary pads" bure kwa wanawake wa vyuo vikuu na sehemu zingine zenye lockdown.

Nafikiri kuna kama myth kwa wanaume, kuwa Hedhi salama ni jambo la mwanamke pekee na sisi wanaume halituhusu kabisa, kwa kufikiria tu hivyo moja kwa moja , inatunyima nafasi kuongea kwa uwazi kuwatetea wanawake katika suala la upatikanaji wa vifaa salama na bei nafuu au bure, wanapokuwa wanapitia katika kipindi cha hedhi.
Huwa napitia maumivu ambayo wengi wa wazazi huwa hawayajali na kulazimisha kufanya kazi mbalimbali za nyumbani nikiwa siko vizuri. Bei ya taulo za kike iko juu kiasi kwamba inakuwa si rahisi kugharamikia muda mwngine nikiwa katika hedhi
Hedhi salama imekuwa ikizingatiwa zaidi maeneo ya mjini ambako miundombinu ni mzuri na kusahaulika katika maeneo ya vijijini.
Hedhi salama ni haki ya kila msichana na wanawake wote kwa ujumla

Swala la hedhi katika jamii inayotuzunguka inachukuliwa kama jambo la siri hivyo hawaliongelei hadharani maana inaonekana kama ni ukosefu wa maadili na ni kinyume cha mila na utamaduni wetu na pia linaonekana ni kinyume na dini. Licha ya harakati na kampeni nyingi zinazoendelea kuhusu uhamasishaji wa hedhi bado hili swala linapingwa katika baadhi ya maeneo ambaya wanaamini ni swala la siri.
Mazingira salama yapo lakini sio katika maeneo yote ya jamii
Mfano upatikanaji wa sanitary pads kwa maeneo ya vijijini ni changamoto hivyo inawalazimu baadhi ya wasichana wadogo kutumia vitambaa ambavyo vinawafanya wasiwe wanajiamini wakiwa kwenye hedhi
Pia kwa Mazingira ya shule, Ukosefu wa maji katika baadhi ya vyoo vya kwenye mashule ni changamoto kwani maji ni muhimu katika usafi mtu atakapokuwa kwenye hedhi.
Jamii inayonizunguka inachukulia suala la hedhi kama jukumu linalomuhusu mwanamke tuu hvyo wanaume hawashiriki chochte katika kuhakikisha hedhi salama.
Hedhi Salama kwa walemavu.
Kutoka kwa Sophia Mbeyela,
"Kundi la watu wenye ulemavu limegawanyika kwenye namna mbalimbali, mfano viziwi, wasiosikia, na namna nyingine nyingi. atika kila aina ya mlemavu kuna aina inayomfaa ili kumfikishia ujumbe. Unapokosekana uwezo wa kutoa taarifa kwa kundi moja wapo maana yake wasichana au wanawake pia wanakosa taarifa sahihi ikiwemo hii ya hedhi salama. (Gharama kubwa kusaidia kupatikana kwa wakalimani, kutengeneza video maalum kwa ajili ya kutoa taarifa).
Walemavu wengi hupata taarifa kutoka kwa watu wa karibu lakini napo ni changamoto sababu nyingi huwa sio taarifa sahihi na zenye usiri mwingi.
Changamoto ya kimazingira, maeneo yetu mengi mfano mashuleni, makazini, hospitalini hakuna miundombinu mizuri kama milango midogo kwa wheelchair kupita, ngazi nk. kwa walemavu wa aina mbalimbali, kwa hiyo, walemavu hao hupata changamoto ya kufikia maeneo ya kujisitiri kwa ajili ya usafi. Hii hupelekea mlemavu akiwa hedhini kuamua kupumzika nyumbani kwa siku hizo ili ajisitiri nyumbani.
Ukosefu wa maji au umbali wa vyanzo vya maji pia ni changamoto kufikia hedhi salama. Lakini pia gharama za kupata visaidizi kama "sanitary pads" kwa baadhi ya familia ni kubwa kwao. Ukosefu wa lishe bora kwa ajili ya kujenga miili yao kwenye familia duni husababisha ukoseffu wa hedhi salama kwa walemavu.
Janga la #CORONA pia limechangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa hedhi salama kwa walemavu sababu watu wao wa karibu wanaogopa kukaa nao karibu na kuwasaidia kwa kigezo cha kila mmoja kukaa mbalimbali kutoka mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine (social distancing). Kwa sababu hii walemavu hukosa wasaidizi na kupitia kipindi kigumu kujisaidia wao wenyewe.
Tunaposema #LeaveNoOneBehind, sisi kama jamii, kila mmoja kwa nafasi yake tushirikiane kutatua changamoto hizi zote. Gharama zipo tena sana haswa kwa walemavu, wadau na serikali tushirikiane kutatua changamoto na kuketa mabadiliko. Mfano, kuandaa vipeperushi kuhusu hedhi salama ziwekwe kwenye mfumo wa nukta nundu ili ziwafikie na walemavu. Suala la ulemavu sio la kushikiliwa na mlemavu bali na jamii nzima. Ulemavu humpata mtu wakati wowote. Kuwezesha familia za watu wenye ulemavu kiuchumi kusaidia ukuaji wao kifedha waweze kutatua changamoto zao zingine kwa kuwapatia mitaji.
Sisi kama PEACE LIFE DISABILITY FOUNDATION tunapaza sauti ili kutatua changamoto zinazowakumba wenye ulemavu, kutoa taarifa sahihi kwa makundi mbalimbali ya ulemavu na kuwakomboa kifikra na kuwkaumbusha walemavu kuwa na wao wana uwezo wa kufikia ndoto zao.
Kutoka kwa Sophia Mbeyela,
"Kundi la watu wenye ulemavu limegawanyika kwenye namna mbalimbali, mfano viziwi, wasiosikia, na namna nyingine nyingi. atika kila aina ya mlemavu kuna aina inayomfaa ili kumfikishia ujumbe. Unapokosekana uwezo wa kutoa taarifa kwa kundi moja wapo maana yake wasichana au wanawake pia wanakosa taarifa sahihi ikiwemo hii ya hedhi salama. (Gharama kubwa kusaidia kupatikana kwa wakalimani, kutengeneza video maalum kwa ajili ya kutoa taarifa).
Walemavu wengi hupata taarifa kutoka kwa watu wa karibu lakini napo ni changamoto sababu nyingi huwa sio taarifa sahihi na zenye usiri mwingi.
Changamoto ya kimazingira, maeneo yetu mengi mfano mashuleni, makazini, hospitalini hakuna miundombinu mizuri kama milango midogo kwa wheelchair kupita, ngazi nk. kwa walemavu wa aina mbalimbali, kwa hiyo, walemavu hao hupata changamoto ya kufikia maeneo ya kujisitiri kwa ajili ya usafi. Hii hupelekea mlemavu akiwa hedhini kuamua kupumzika nyumbani kwa siku hizo ili ajisitiri nyumbani.
Ukosefu wa maji au umbali wa vyanzo vya maji pia ni changamoto kufikia hedhi salama. Lakini pia gharama za kupata visaidizi kama "sanitary pads" kwa baadhi ya familia ni kubwa kwao. Ukosefu wa lishe bora kwa ajili ya kujenga miili yao kwenye familia duni husababisha ukoseffu wa hedhi salama kwa walemavu.
Janga la #CORONA pia limechangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa hedhi salama kwa walemavu sababu watu wao wa karibu wanaogopa kukaa nao karibu na kuwasaidia kwa kigezo cha kila mmoja kukaa mbalimbali kutoka mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine (social distancing). Kwa sababu hii walemavu hukosa wasaidizi na kupitia kipindi kigumu kujisaidia wao wenyewe.
Tunaposema #LeaveNoOneBehind, sisi kama jamii, kila mmoja kwa nafasi yake tushirikiane kutatua changamoto hizi zote. Gharama zipo tena sana haswa kwa walemavu, wadau na serikali tushirikiane kutatua changamoto na kuketa mabadiliko. Mfano, kuandaa vipeperushi kuhusu hedhi salama ziwekwe kwenye mfumo wa nukta nundu ili ziwafikie na walemavu. Suala la ulemavu sio la kushikiliwa na mlemavu bali na jamii nzima. Ulemavu humpata mtu wakati wowote. Kuwezesha familia za watu wenye ulemavu kiuchumi kusaidia ukuaji wao kifedha waweze kutatua changamoto zao zingine kwa kuwapatia mitaji.
Sisi kama PEACE LIFE DISABILITY FOUNDATION tunapaza sauti ili kutatua changamoto zinazowakumba wenye ulemavu, kutoa taarifa sahihi kwa makundi mbalimbali ya ulemavu na kuwakomboa kifikra na kuwkaumbusha walemavu kuwa na wao wana uwezo wa kufikia ndoto zao.
![]() |
Sophia Mbeyela, mwanzilishi wa PEACE LIFE DISABILITY FOUNDATION, akipaza sauti kwa ajili ya kuhakikisha kufikiwa kwa hedhi salama kwa wasichana walemavu kwenye ukurasa wake wa twitter. |
Kila Jambo lina changamoto kubwa katika mtu binafsi kulitatua lakini umoja wa mashirikiano unatoa majibu kwa urahisi na yenye uhakika.
ReplyDeleteHedhi Ni Jambo ambalo pengine si kubwa kufadhaika lakini Ni hatari pale ambapo linakuwa tatizo lisilotafutiwa ufumbuzi kwa mabinti wadogo walioko mashuleni Mimi Ni mwanaume lakini sikuona aibu pindi mdogo wangu wa kike anapopata hali Kama hiyo kutaka kujua siku zake ili kumuandalia mazingira ya kupata pedi maana Ni wanawake wachache wanaoweza kumuamba jinsi Me akiwa katika hali hiyo.
Kuna makundi mengi ambayo yanahitaji uhisani wa wadau , serikali na watu binafsi kutetea ili wapate nafuu ya kupata pedi bure na kuendelea na shughuli zao bila tabu ya kukosa uhuru.
1.WANAFUNZI
Pengine ndo kundi kubwa la wahanga hasa walioko vijijini kwani maisha ya kuelewa Jambo hili Ni gumu Sana lakini ata jamii haitilii maanani Sana kwani mabinti wengi huvunja ungo ingali wako shule za msingi na hupitia wakati mgumu kupata hifadhi ya usalama wao pindi wanapoingia kwenye siku zao lakini Ni janga mpaka sekondari hushindwa kupata pedi. Ni wajibu wa serikali kupeleka kila shule za kata Pedi za bure kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike hali hii inaweza ata kumkosesha mitihani muhimu mtoto wa kike Ni vema Sasa kupitia sera na limekuwa halionekanj tatizo kwasababu watunga sera na Sheria mbali mbali Ni wanaume halitutokei sisi ndo maana tumelichukulia kawaida Ni mda wa kubadili fikra zetu kuvaa viatu vya mabinti wetu.
2.WALEMAVU NA WENYE UPUNGUFU W AKILI.
Ni Jambo najiuliza kila siku he hawa msaada wanaopata unatoka wapi kwani wapo mabinti wenye upungufu wa akili wanapatwa na hali hii Kama wapo watu wanaowapa mimba kwanini wasiwepo watu wa kuwastili katika hali zao za kupata hedhi kumbe ukichaa si kugeuka mbuzi unabaki na hali ya ubinadamu Ni vema serikali kuwakusanya watu wenye upungufu wa akili hasa wanawake kuwasidia katika Jambo hili kwani nimekutana na story ya binti mmoja watu wanasimuliana Kam Jambo zuri kwamba "has yule damu zinamtoka mpaka zinakauka zenyewe je " ingekuwa mama yako usingechukua hatua kumtoa kwenye udhalilishaji huo.
Lakini pia walemavu wanastahili kusaidiwa maana hawatoki na wapo wengine hawawezi kuongea Ni vema serikali kupitia viongozi wa mtaa kutambua kil nyumba Kuna mabinti wangapi wanaulemavu na wanakumbukwa katika kupata mahitaji ya hedhi salama.
( Swanaume tuanze kuchukua jukumu la kusaidia mabinti na wanawake wote kupata #HedhiSalama si aibu ni hali ya kusaidiana na upendo pia.)
Asante sana kwa mchango!
Delete